HAITOKEI VIZURI? ITAZAME KWENYE KIVINJARI

+254 (0) 735 195 116

WanWaks® Hosting

KAMPUNI MATHUBUTI YA UVUZI

Kiswahili | English

UVUZI NAFUU KABISA BARANI HUU HAPA!

WanWaks® Hosting inaendelea kuwapa wateja wake huduma bora ya uvuzi (hosting) wa tovuti kwa utandawazi pahali popote ulipo eneo la Afrika Mashariki na Kati na tungependa kukuhusisha wewe au biashara yako kwenye ufanisi wetu.

Jee? Ungependa kuimiliki au unapangia biashara yako kuwa na anwani ya barua pepe ya kibinafsi isiyo ya gMail au yahoo ama yeyote ile ya sare unayoitumia kwa sasa? Unataka kuonekana mtaalam thabiti au kujitenga na wenzako wanaosalia baghala? Unaweza kuipata sasa kwa Ksh. 950 au $ 12 kwa mwaka na mpango wetu mdogo zaidi wa Chiriku.

MENGINE ?

WanWaks® Hosting utakuunganishia akaunti yako uliyo nayo kwa sasa ya gmail, yahoo au ya huduma yeyote ile ya sare na akaunti yako taalam ya kibinafsi ili tuu usipoteze anwani zako kwa ghafla.

Habari njema ni, tunakufanyia SARE !

Jee, ungependa pia kujua ni watu wangapi huizuru tovuti yako kila siku ya wiki au hata idadi jumla kwa mwezi?

Usijali !

WanWaks® Hosting huripoti takwimu hizi kwa wateja wake kila mwezi au wakati wowote ikihitajika bila malipo yeyote. Hivyo,

Usipoteze fursa hii ya kipekee ya kufuatilia mienendo na matumizi ya tovuti yako mtandaoni.

WanWaks® Hosting pia inawapa fursa wa kuchagua mpango wa kuvuza unaokufaa zaidi kwa kuhakikisha kua kuna mipango mbalimbali kuanzia ya bei nafuu kwa wateja ibuka au wadogo hadi yenye nguvu zaidi kwa wateja mashuhuri na wenye mahitaji shamiri. Haya mipango yametajwa baada ya ndege maridadi wakiwemo ndege tajika wanaoibukia milimani, visiwani na hata nyika za bara Afrika. Chaguo ni lako, Jishindie ndege wako sasa!

TAZAMA YAFUATAYO

MIPANGO YETU YA UVUZI

Chiriku (Ksh.950 | $ 12)

Kwa Mwaka

Chiriku inawafaa kwa sana watu binafsi, wanasiasa chipukizi, wanafunzi ama biashara ambazo tovuti zao hazina shughuli kibao. Yaani zisizo pokea zaidi ya wageni 20 kwa mwezi.

Aidhaa kama ungependa kuvuza tu anwani binafsi ya barua pepe basi Chiriku ndio ndege atakaye rahisisha mambo yako. Mpango huu una hifadhi ya 1GB.

get This Bird

Njiwa (Ksh.1,999 | $ 24)

Kwa Mwaka

Njiwa ni ndege anayesifika kwa kuwa mpole na asiye na shughuli nyingi na kwa sababu hii, mpango wa Njiwa ni wa  tovuti ambazo zinapokea wageni kati ya 20 hadi 50 kwa mwezi.

Pia kama ungependa kuwa na uwezo wa kutuma barua pepe kwa wingi Njiwa ni ndege wa kutegemewa. Mpango mzima wa Njiwa una hifadhi ya 2.5GB na unao uwezo wa kushughulikia watumiaji wengi iwezekanavyo.

get This Bird

Kipanga (Ksh.3,999 | $ 49)

Kwa Mwaka

Kipanga ni ndege wa kimo cha wastani na mwenye makali mengi.

Kama mpango wa uvuzi, makali yake yanaelekezwa kuwapokea na kuhudumia wageni zaidi ya 100 wanao itembelea tovuti zenye shughuli nyingi kiasi na kutuma barua pepe kwa wingi.

get This Bird

Kasuku (Ksh9,999 | $ 117)

Kwa Mwaka

Kasuku ni ndege wa shughuli nyingi na maneno mengi na ili kuwezanaye lazima mja aweze kumpa nafasi kubwa.

Mpango wa Kasuku basi ni mpango wa kampuni za kimo cha kadri na ambazo hupokea wageni zaidi ya 200 kwenye tovuti zao. Mpango huu pia unawafaa wasaani na wanasiasa wenye mashabiki wengi, shule, hosipitali na kadhalika.

get This Bird

Tai (Ksh.19,950 | ($ 239)

Kwa Mwaka

Tai ni mpango wa WanWaks® Hosting wa juu zaidi. Unazifaa kampuni kubwa na mashirika makubwa ambazo tovuti zao hupokea zaidi ya wageni 500 kwa mwezi.

Hifadhi na ufurushi wa data haina kipimo ndani ya mpango huu. Kwa kina zaidi inafaa bodi za serikali, Kampeni za barua pepe, kampuni za habari au mtandao na utaraki mathubuti.

get This Bird

Mbona WanWaks® Hosting

Ununuzi wa mipango yetu ya WanWaks® Hosting ni otomatiki na imewezeshwa pamoja na njia mbambali uzipendazo za kutuma na kupokea pesa kwa mtandao kama vile Mpesa, Airtel Money, Pay Pal, MasterCard, Visa Card, Pesa Pay na kadhalika.

Zaidi ya hayo;

 • Msaada wa masaa 24/7 mwakani na wahudumu waliokita mizizi katika fani hii ya uvuzi na utandawazi kwa ujumla.
 • Uhakika wa 100% wa kuregeshewa fedha.
 • Hifadhi kubwa na ufurushi mkubwa wa data popote ulipo.
 • Seva mathubuti inayohakikisha 99.99% ya kuweko hewani.
 • Anwani za baruapepe na akaunti za FTP visivyo na kipimo.
 • Kuunganishiwa akaunti yako mpya ya kibinafsi ya barua pepe na uliyo nayo kwa sasa ya gmail au yahoo au ya huduma yeyote ile bila malipo ya ziada.

cPanel zetu zinauwezo wa kusitiri mitindo mipya ya kutaraki(computing) za kisasa ikiwemo lugha za tarakimu ibuka na mfumo wa kukatibu data (CMS) uipendayo.

 • Uvuzi wa Word Press, Joomla, Magento, Drupal na kadhalika.
 • Uvuzi wa barua pepe
 • Vipengee vya Domain/FTP
 • eCommerce
 • Takwimu za Tovuti
 • Vipengele vya utaraki (Scripting features)

WanWaks® Hosting pia husajili anwani za tovuti za humu nchini na za kimataifa kwa bei nafuu kwa mwaka. Bonyeza hapa kujifunza zaidi.

Help Line

Help Line

Help Line

Wahudumu wetu wanasubiri kwa hamu na gamu. Wafikie kwa wakati wowote masaa 24/7 mwakani kubaini zaidi ili ujishindie ndege wako sasa! Tuma barua pepe kwa

vipi@wanwaks.com

au piga simu kwa nambari

+254 (0) 735 195 116

HAITOKEI VIZURI? ITAZAME KWENYE KIVINJARI

MASWALI NA MAJIBU | SERA ZA FARAGHA | KAMPUNI | vipi@wanwaks.com | vipi@wanwaks.com | www.msoomi.systems